nimependezwa sana na huu utaratibu wa kujivua gamba unaoendelea nchini kwetu Tanzania. ni jema kwa viongozi wazalendo kujivua madaraka pale wale wanaowaongoza wanapo poteza imani nao.
tunategema kwamba viongozi hawa wanaochukua uamuzi huu mzuri wa kujivua madaraka wawewatulivu badala ya kuona kwamba wanaonewa. pia ni jambo la msingi mahakama ikawa hujru kwa kutoa haki pale wananchi wanapodhulumiwa au viongozi kuonewa, na pia baada ya hawa wazee wetu kujitoa madarakani waungane na wananchi katika kuwafichua wengine ambao wanalifanyia taifa ndivyo sivyo tena kwa amani bila ya hila wala kinyongo.
kuacha uongozi kutokana na tuhuma za wazi ni uzalendo lakini nini mwisho wake,
No comments:
Post a Comment