Saturday, April 7, 2012

KANUMBA KATUTOKA

Steven Kanumba amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa Muhimbili. Habari zaidi zitawajia baadae

No comments:

Post a Comment