Monday, February 7, 2011

WANAFUNZI VYUO VIKUU

Tanzania haina hela ya kuwawezesha wanafunzi vyuo vikuu kuendelea na masomo kwa kuwapa mikopo kwa muda, lakini hela za DOWANS zipo, heri wananchi waumia kwa kulipa kodi, bidhaa kupanda bei ilimradi DOWANS ilipwe. Tanzania kila siku tunalalamika misaada, yanini kama mnapigania mamilioni ya Rostam na interest zake pamoja na mabilion ya DOWANS?

SWALI

Maandamano TZ yanaleta mabadiliko? au watu wanachomwa na jua wengine kuambulia vilema kutokana na kupigwa na police,? kwani watu kudai haki zao wanazuiliwa, ina maana kuna wenye haki zaidi ya wengine? kwanini ktk maandamano Arusha Dr Slaa na Ndesamburo walikamatwa wakafungiwa ndio kichapo kikatembea sio kwamba waliwahifadhi? au wanaogopa kuwavunja mikono kama walivyo fanya kwa Lipumba? tufikirie njia nyingine ya kudai haki zetu vinginevyo wananchi tutaangamia huku wakubwa wetu wakilindana;